Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: vikwazo na mzingiro mkali unaofanywa na jeshi la Syria na washirika wake dhidi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh linaloungwa mkono na Marekani na washirika wake, vimepelekea kulilazimisha kundi hilo la kigaidi kuwaachia huru mamia ya raia waliowatumia kama ngao ya binadamu wakati wakiikimbia ngome yao kaskazini mwa Syria,lakini hatima ya wengine haijulikani tangu jana Jumamosi tarehe 13 mwezi wa 8 mwaka 2016.
Katika eneo jingine, wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh kadhaa waliuwawa jana Jumamosi katika shambulio la ndege za kijeshi za jeshi la serikali ya Syria pamoja na washirika wao wa Urusi, ambapo magaidi hao walijibu mashambulizi kwa kuwaua raia wasio na hatia na katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh katika eneo la mapigano katika jimbo la Aleppo, limesema kundi linaloangalia hali nchini humo.
Kiasi ya raia 51 ikiwa ni pamoja na watoto waliuliwaa na magaidi hao mjini Aleppo na linalozunguka mji huo, wakati raia wengine 22 waliuwawa katika jimbo jirani la Idlib, shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria limesema.
Wapiganaji wa mwisho wa kundi la kigaidi la Daesh walikimbia kutoka mji wa Manbij karibu na mpaka na Uturuki siku ya Ijumaa baada ya kushambuliwa vikali na majeshi ya Syria yakishirikiana na majeshi ya Iran,
wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon kusema inaonekana kuwa wapiganaji hao wa kigaidi wameelemewa na majeshi ya serikali.
Kukimbia kutoka mji huo ambao ulikamatwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh mwaka 2014 ilikuwa pigo kubwa kabisa kwa magaidi hao wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake.
Magaidi bado wanatumia Ngao ya binadamu
wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh waliokimbia waliondoka pamoja na kiasi ya raia 2,000, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, siku ya Ijumaa kuzuia mashambulizi ya anga wakati wakielekea katika mji wa mpakani unaoshikiliwa bado na kundi hilo wa Jarabulus, kwa mujibu wa wapiganaji hao wa SDF.
Kiasi ya baadhi ya watu waliochukuliwa na wanamgambo hao baadaye waliachiliwa ama walitoroka, jana Jumamosi, lakini haijulikani watu wengine wako wapi.
"Hakuna wapiganaji tena wa kundi la kigaidi la Daesh " waliobakia mjini Manbij, mwanajeshi mmoja wa Syria alisema.
Televisheni ya Wakurdi ilionesha picha za raia wakifurahia mjini Manbij, ikiwa ni pamoja na akina mama waliokuwa wakitabasamu, ambao waliondoa hijabu zao na wanawake waliwakumbatia wapiganaji wa Kikurdi.
Mwanamke mmoja alichoma nguo nyeusi ambayo wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wanaodhamini wa na Marekani na Saudia arabia waliwalazimisha wakaazi kuvaa, wakati wanaume ambao waliishi kwa wiki kadhaa wakilazimishwa kuacha ndevu zao bila kuzinyoa , walizinyoa.
Mabomu kila nyumba
"Mapambano yalikuwa makali," duru kutoka kwa wakurdi zimezungumza na shirika la habari la afp, na kuongeza wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh waliweka mabomu katika mji huo.
"Mmoja kati ya wapiganaji wa SDF aliingia katika nyumba siku ya Ijumaa na kuona magaidi hao wanaodhaminiwa na Saudia arabia wameweka kiatu juu ya kitabu kitukufu cha Kuran. Alipokiondoa kulikuwa na mripuko na aliuwawa," duru hiyo ilisema.
Mkaazi mmoja aliliambia shirika la habari la afp hakukuwa na hata nyumba moja katika eneo anakoishi ambalo halikutegwa mabomu.
"Tunawaomba watu wanaohusika kuchukua hatua" ya kuyaondoa mabomu hayo, Jamal Abul Ababiyya alisema, na kuongeza kwamba mabomu yanawajeruhi watu kila siku.
Picha za shirika la habari la afp zinaonesha mitaa ya mji huo ikiwa imetapakaa taka na ukuta bado ukiwa umechorwa bendera ya wapiganaji hao wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh yenye rangi nyeusi na nyeupe.
Majeshi ya Syria yakishirikiana na majeshi ya Iran na Urusi yanaendelea kuwaangamiza wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo licha kukwamishwa na Marekani na washirika wake wanaunga mkono magaidi hao.
Mwisho wa habari/ 291