Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: serikali y a Markani imeendelea kuwapatia silaha wapiganaji wa kikurdi na kuwahamasisha wapambanane na wanajeshi wa Serikali ya Syria.
Wapiganaji wa Kikurdi kaskazini mwa Syria wametolea mwito wapiganaji wa jeshi la Syria wanaopambana na magaidi wa Daesh kuweka chini silaha zao na kujisalimisha kufuatia wapiganaji hao wa kikurdi kupiga hatua katika mji wa Hassakeh
"Kwa wanamgambo wote wa serikali waliyozingirwa, sasa mnalengwa na vikosi vyetu, walenga shabaha na silaha zetu,” kilisema kitengo cha ulinzi wa raia nchini Syria YPG. “Hatutarejea nyuma, vikosi vyetu vinaelekea mjini, tunawatolea mwito muweke silaha chini na kujisalimisha katika makao makuu ya usalama yaliyoko karibu nanyi,” kiliongeza kitengo hicho cha ulinzi wa raia. Cha kikurdi kinacho dhaminiwa na Marekani.
Maeneo mengi ya mji wa Hassakeh yanakaliwa na vikosi vya YPG wanaodhaminiwa na Marekani lakini vikosi vya rais Bashar al Assad na wanamgambo waliyotiifu kwa serikali wanaendelea kudhibiti baadhi ya maeneo ya mji huo. Idriss Nassan, afisa mkuu wa Wakurdi amesema kundi hilo limechukua udhibiti wa maeneo mengi mjini humo hasa katika eneo jirani Ghwarian na baadhi ya miji ya mashariki ya Nashwa na al -Hassakeh. Hata hivyo, bado mapigano makali yameripotiwa kuendelea katika maeneo hayo.
Wiki iliyopita ndege za kivita za serikali ya Syria zilivurumisha mabomu kwenye ngome zinazoshikiliwa na wakurdi wanaotumwa na Marekani mjini al Hassakeh kwa mara ya kwanza katika historia ya vita hivyo vinavyochochewa na Marekani nchini humo vinavyoendelea kwa miaka mitano sasa. Mapigano yalipamba moto kati ya vikosi vilivyotiifu kwa serikali na wanajeshi wa Kikurdi, wanaoungwa mkono na Marekani katika. Aidha Marekani imetoa onyo kwa serikali ya Syria kutoyashambulia makundi ya kigaidi inayoyaunga mkono kwa ndege za kivita. Nayo Urusi imeahidi kuwa bega kwa bega na Syria katika kupinga njama hatari za Marekani na washirika wake za kutaka kuigawa Syria.
Wakurdi wanaochangia silimia 10 ya raia wa Syria milioni 22.4 kabla ya vita, wamekuwa wamekuwa wakiatumiwa na Marekani kuwashambulia wanajeshi wa Serikali ya Syria
Kwa upande mwengine Uturuki, inawatumia magaidi wa Daesh kuwaua raia wa kikurdi wanaoishi Syria na Uturuki huku Marekani ikiwatumia magaidi hao kupambana na majeshi ya Syria katika malengo yake hatari ya kuangusha serikali halali ya Syria kama walivyofanya kwa serikali ya Gaddafi wa Libya. Kwa sasa Uturuki imeridhia kikundi cha kigaidi kinachoojiita jeshi huru la Syria kujikusanya katika ardhi yake ili kushambulia kijiji kinachoshikiliwa na wanamgabo wa kundi la kigaidi la Daesh ambao walikuwa washirika wa karibu wa Uturuki kabla ya kuasi, kwa lengo la kuwanyima nafasi au udhibiti kundi la YPG la wakurdi linadhaminiwa na Marekani.
Mwisho wa habari/ 291