Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Makundi ya magaidi wa Syria yaliyovunjika yanapanga kuanzisha mashambulizi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh linaloungwa mkono na Marekani, kwa lengo la kuwaondoa katika ardhi ya nchi hiyo wakisaidiana na serikali ya Uturuki. Magaidi hao wakiwemo wa Daesh wana lengo la kuishambulia Jarablus ikiwa ni mji mkuu wa mwisho mpakani mwa Uturuki unaoshikiliwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh. Kundi hilo la Daesh limepoteza udhibiti wa maeneo kaskazini mwa Syria kwa kundi la wapiganaji wa kikurdi wa YPG wanaoungwa mkono na Marekani ambalo Marekani analitumia kundi hilo kupambana na serikali ya Syria.
Mwishoni mwa juma, Waziri Mkuu Binal Yildrim alisema Uturuki itakuwa na "kibarua zaidi" nchini Syria katika miezi ya hivi karibuni pasipo kuweka wazi mipango yoyote. Naye, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, amesema hii leo kwamba mipaka ya Uturuki ni lazima "isafishwe" dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh ambalo kwa muda mrefu limekuwa likitumiwa na Marekai na washirika wake kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syria.
Mwisho wa habari/ 291