24 Agosti 2016 - 21:45
Jeshi la Uturuki laingia Syria bila idhidi ya serikali

serikali ya Uturuki imepeleka vifaru katika mji wa Jarablus Kaskazini mwa Syria katika kile inachodai kuwa ni operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh, ambalo hapo awali lilikuwa na uhusiano wa karibu na Uturuki, Hayo yanajiri wakati Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden akianza ziara nchini Uturuki.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: serikali ya Uturuki imepeleka vifaru katika mji wa Jarablus Kaskazini mwa Syria katika kile inachodai kuwa ni operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh, ambalo hapo awali lilikuwa na uhusiano wa karibu na Uturuki, Hayo yanajiri wakati Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden akianza ziara nchini Uturuki.

Ripoti ambazo zimezinukuu duru za kijeshi, zimesema operesheni hiyo ya jeshi la Uturuki iliyopachikwa jina la ''Ngao ya Euphrates'' imeanza leo kabla ya mapambazuko. Serikali ya Uturuki imesema operesheni hiyo inasaidiwa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi kundi hilo la kigaidi. Makundi kadhaa ya magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na Uturuki wa Syria hali kadhalika yamesema yameingiza wapiganaji wao katika mji wa Jarablus, kupambana na magaidi wa Daesh.

Akizungumza muda mfupi uliopita mjini Ankara, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amethibitisha kuanza kwa operesheni hiyo, na kuongeza kuwa nchi yake inaazimia kuhakikisha wasyria wanakuwa na udhibiti wa nchi yao wenyewe. Erdogan amesema ikiwa lazima, Uturuki itajitwisha jukumu la kuhakikisha kuwa azma hiyo inafikiwa.

Operesheni yashirikisha muungano unaoongozwa na Marekani

Awali ofisi ya waziri mkuu wa Uturuki imesema operesheni ''Ngao ya Euphrates'' ambayo ndio kubwa zaidi kuwahi kufanywa na Uturuki nchini Syria inashirikisha vikosi vya anga na vya nchi kavu, na kwamba shabaha yake ni kuukomboa mji wa Jarablus kutoka mikononi mwa makundi yamagaidi hao hatari. Mji huo uko kwenye mpaka baina ya Uturuki na Syria.

Ndege za jeshi la Uturuki chapa F-16 na nyingine za muungano unaoongozwa na Marekani zimepiga maeneo kadhaa ndani ya Syria, na mpiga picha wa shirika la habari la AFP ameshuhudia msafara wa vifaru vya Uturuki ukivuka mpaka kuingia Syria.

Wakati huo huo makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden amewasili leo nchini Uturuki, ikiwa ziara ya kwanza ya kiongozi wa ngazi ya juu wa wa nchi ya Magharibi kuizuru Uturuki, tangu kushindwa kwa jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wa rais Erdogan, hapo Julai 15.

Muungano unaoongozwa na Marekani kwa madai ya kupambana na kundi la kigaidi la Daesh, mara kadhaa wakadhaa umelaumiwa kwa kuwasaidia magaidi badala ya kuwashambulia.

Biden awasili kupunguza mvutano

Biden atataka kupunguza mvutano kati ya nchi yake na Uturuki ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami, NATO, hususan kuhusu kuwepo nchini Marekani kwa Ulamaa wa Kituruki Fethullah Gulen, ambaye utawala wa Rais Erdogan unamtuhumu kuwa kinara wa jaribio la mapinduzi lililoshindwa.

Uturuki imekuwa ikiishinikiza Marekani kumrejesha nyumbani Gulen ambaye anakanusha vikali kuhusika kwa njia yoyote ile na jaribio hilo.

Tofauti nyingine kubwa kati ya Uturuki na Marekani ni kuhusu kundi la wanamgambo wa Kikurdi la YPG, ambalo linachukuliwa na Uturuki kama kundi la kigaidi, wakati Marekani ikilichukulia kama mshirika muhimu katika vita vya Syria na inalipambana na majeshi ya Syria ili kuangusha serikali ya Bashar asad.

Katika operesheni yake ya kijeshi nchini Syria, Uturuki inakusudia kuonyesha kuwa haina mzaha katika kulishughulikia kundi la kigaidi la Daesh, ambalo limeshutumiwa kufanya mashambulizi kadhaa ya kigaidi nchini Uturuki, likiwemo la Jumapili iliyopita lililouwa watu 54 waliokuwa kwenye sherehe za arusi katika mji mwingine wa mpakani wa Gaziantep.

Mwisho wa habari/ 291