Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Muhammad al Houthi amesema leo kwamba, wananchi wa Yemen hawatasalimu amri mbele ya wavamizi na kadiri mashambulizi ya Saudia yanavyoshtadi dhidi ya wananchi wa Yemen ndivyo nao pia wanavyozidi kuwa imara na kuzidisha muqawama dhidi ya wavamizi wa nchi yao.
Al Houthi amesema kuwa, kombora ambalo siku ya Jumatatu liliilenga taasisi ya Shirika la Mafuta la Saudi Arabia (ARAMCO) liliundwa Yemen kwa asilimia mia moja na kuongeza kuwa: Kombora hilo la Yemen ambalo limeuvuka mfumo wa ulinzi wa makombora wa Saudia linatoa ujumbe huu kwa watawala wa Saudia kwamba: Rudini tena kwa Marekani na mnunue mfumo mpya wa ulinzi wa anga."
Kikosi cha makombora cha vikosi vya ulinzi vya Yemen alfajiri Jumatatu kilikipiga kituo cha usambazaji cha Shirika la Mauta la Saudi Arabia la Aramco kwa kutumia kombora lenya mabawa aina ya Quds-2 huko katika mji wa Jeddah.
Saudi Arabia mwezi Machi mwaka 2015 iliivamia kijeshi nchi maskini ya Kiarabu ya Yemen kwa kuungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi nyingine kadhaa na kisha kuizingira nchi hiyo kwa upande wa majini, angani na nchi kavu.
342/