ABNA24 : Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria jana usiku ilitoa taarifa na kulaani hatua ya Trump ya kutambua rasmi mamlaka ya Morocco huko Sahara Magharibi na kueleza kuwa, uamuzi huo wa Trump hauna uhalali wowote wa kisheria na ni kinyume na maazimio yote ya Umoja wa Mataifa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria imesisitiza katika taarifa yake kuwa: mzozo wa eneo la Sahara Magharibi utapatiwa ufumbuzi kupitia tu sheria za kimataifa na jitihaa za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Kuhusu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Morocco na utawala wa Kizayuni Abdelaziz Djerad Waziri Mkuu wa Algeria amesema: utawala huo upo katika mipaka ya Algeria; na tunapasa kuwa wamoja ili kukabiliana na tishio hilo.
Donald Trump Alhamisi iliyopita alitangaza kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba: Mfalme wa Morocco na Israel zimefikia mapatano ya kuanzisha uhusiano kamili kati yao. Trump aidha aliandika kuwa: Marekani inatambua rasmi mamlaka ya Morocco kwa eneo la Sahara Magharibi.
Wakati huo huo, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa mapatano hayo hatari ni sawa na zawadi ya bure ambayo tawala za Kiarabu zimeupatia utawala wa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya Wapalestina.
342/