9 Januari 2021 - 14:49
Mgogoro jeshini Israel, wanajeshi elfu 10 wawekwa karantini

Duru za utawala wa Kizayuni zimetangaza habari ya kuongezeka vibaya maambukizo ya kirusi cha corona ndani ya jeshi la utawala huo dhalimu na kusema kuwa maelfu ya wanajeshi wa Israel wamewekwa kwenye karantini hivi sasa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mtandao wa Walla News wa utawala wa Kizayuni umetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, idadi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliokumbwa na kirusi cha corona imeongezeka sana kiasi kwamba katika kipindi cha siku mbili tu zilizopita, wanajeshi 167 wa Israel wamepatwa na ugonjwa hatari wa COVID-19.

Mtandao huo umesisitiza kuwa, sehemu kubwa ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wako kwenye karantini katika sehemu zao za kazi na kuongeza kuwa, idadi ya wanajeshi wa Israel wanaowekwa kwenye karantini itakuwa kubwa zaidi katika siku zijazo.

342/