Jens Larke, msemaji wa OCHA, amesema: "Umoja wa Mataifa una karibu vifurushi 180,000 vya msaada wa chakula na vitu vingine muhimu viko tayari kuingia Gaza."
Larke aliongeza: "Gharama ya bidhaa hizi imelipwa na wafadhili wa kimataifa na ushuru wa forodha. Msaada huu uko tayari kusafirishwa, na tunaweza kuuleta Gaza mara moja na kwa kiwango kikubwa.
Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) amesisitiza kwamba, Ukanda wa Gaza kwa sasa ndilo eneo lenye njaa kubwa zaidi duniani na kuonya kwamba: "Wakati unapotea kwa kasi na maisha ya binadamu yanachukuliwa kila saa."
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Philippe Lazzarini Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa kuzingirwa eneo hilo na utawala wa Kizayuni kunakwamisha misaada ya kibinadamu kuingia katika hilo; kwa hiyo wakazi wa eneo hilo wapo kwenye ukingo wa njaa.
Wakati huo huo, Mfuko wa Kuwahudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeitaja hali ya Gaza kuwa "ya maafa" na kutahadharisha kuwa kizazi chote kinakabiliwa na hatari ya kupoteza usalama, afya, elimu na matumaini.
342/
Your Comment