30 Mei 2025 - 22:21
Source: Parstoday
Vikosi vya Yemen vyashambulia uwanja wa ndege Israel kwa kombora la kasi ya juu

Vikosi vya kijeshi vya Yemen vimeendesha operesheni nyingine dhidi ya utawala dhalimu wa Israel, kwa kulenga Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion kwa kombora la kasi ya juu (hypersonic) ikiwa ni jibu kwa mashambulizi ambayo Israel inaendeleza dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Akizungumza Alhamisi, Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji wa majeshi ya Yemen, amesisitiza kwamba, Yemen itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kidini, kimaadili na kibinadamu kwa watu wa Palestina hadi wakati ambapo hujuma za Israel zitakomeshwa na mzingiro dhidi ya Gaza kuondolewa.

Jenerali Saree alionya kuwa Majeshi ya Yemen hayatasita kujibu mashambulizi yoyote kutoka kwa Israel dhidi ya taifa hilo kwa mashambulizi ya kisasi, ikiwemo marufuku ya usafiri wa anga kwenda na kutoka Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion.

Katika hatua ya kijeshi ya kimkakati, Yemen imeweka mzingiro dhidi ya njia muhimu za anga na baharini za Israel, kwa lengo la kuzuia usambazaji wa vifaa vya kijeshi kwa utawala huo unaoendeleza vita vya mauaji ya kimbari huko Gaza.

Jenerali Saree ameongeza kuwa Majeshi ya Yemen yataendelea na mashambulizi ya kisasi dhidi ya utawala wa Kizayuni hadi ndani kabisa ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina, na kwamba mashambulizi hayo yatazidi kuongezeka kwa kasi.

Amesisitiza  kuwa Yemen haitasitisha operesheni zake za kijeshi hadi pale ambapo uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza utakaposimamishwa kikamilifu, na mzingiro mkali unaoitesa Gaza kuondolewa bila masharti.

Majeshi ya Yemen yametangaza bayana kuwa hayatositisha mashambulizi yao hadi Israel itakapositisha kabisa mashambulizi ya ardhini na ya angani dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Tangu kuanza kwa mashambulizi makubwa ya utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 2023, hadi Jumatano tarehe 28 Mei 2025, ikiwa ni siku ya 600 ya vita, maisha ya kiraia katika eneo hilo yameporomoka kabisa chini ya mashambulizi yasiyokoma ya Wazayuni.

Kwa mujibu wa ripoti huru na mashirika ya kimataifa, zaidi ya Wapalestina 54,000 wameuawa katika mauaji ya kimbari yanayoendelezwa na utawala katili wa Israel, huku wengine 123,000 wakijeruhiwa, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee. Hii ni hali ya janga la kibinadamu lisilo na mfano wake, likiendelea mbele ya macho ya dunia nzima.

Your Comment

You are replying to: .
captcha