1 Juni 2025 - 23:07
Israel yazuia kuingizwa kwa chanjo muhimu kwa watoto wa Gaza

Mkuu wa kitengo cha watoto katika Hospitali ya Nasser Mjini Khan Younis alitangaza kuwa wavamizi wanazuia kuingia kwa chanjo maalum za watoto katika Ukanda wa Gaza.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Mkuu wa kitengo cha watoto katika hospitali ya Nasser mjini Khan Yunis alitangaza kuwa wavamizi wa Kizayuni wanazuia kuingia kwa chanjo maalum za watoto katika Ukanda wa Gaza. 

Taarifa ya hali ya afya ya Gaza – kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kiislamu na mashirika ya kimataifa

Ahmad Al-Farra, katika mahojiano na kituo cha habari cha Al Jazeera, ametangaza kuwa utawala wa Kizayuni umeharibu asilimia 75 ya uwezo wa hospitali katika Ukanda wa Gaza.

Ameongeza kuwa: "Tunateseka kutokana na janga kubwa la kiafya ambalo limewalenga moja kwa moja watoto wa Gaza. Wavamizi wa Kizayuni wanazuia kuingia kwa chanjo maalum za watoto katika eneo hili."

Msemaji wa Hospitali ya Mashujaa wa Al-Aqsa, hapo awali alieleza kuhusu hali mbaya ya mfumo wa afya Gaza, akisema kuwa hadi sasa hakuna dawa wala vifaa vya matibabu vilivyofikishwa katika hospitali za eneo hilo.

Khalil Al-Daqran, katika mahojiano na kituo cha Al-Aqsa, alisisitiza kuwa wavamizi wa Kizayuni wanaendeleza mashambulizi yao bila kujali sheria na mikataba ya kimataifa inayozingatia ulinzi wa vituo vya afya.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, jeshi la Israel limeharibu kabisa Hospitali ya Usadiki ya Uturuki, ambayo ilikuwa maalum kwa ajili ya wagonjwa wa saratani, na pia limelenga kitengo cha dawa za magonjwa ya figo katika Hospitali ya Nasser.

Ametaja hali ya mfumo wa afya Gaza kuwa ni ya “janga kubwa” na ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutekeleza wajibu wao kwa raia wasio na hatia na wagonjwa walioko hatarini.

Shirika la Afya Duniani (WHO) hapo awali lilitangaza kuwa asilimia 94 ya hospitali katika Ukanda wa Gaza zimeathiriwa na mashambulizi ya Israel.

Shirika hilo chini ya Umoja wa Mataifa lilionya kuwa mashambulizi yanayoendelea na mzingiro wa Gaza umesababisha mfumo wa afya kufikia hatua ya kuporomoka kabisa, na wananchi wengi hawawezi tena kupata huduma za msingi za matibabu.

Kwa mujibu wa WHO, kati ya Hospitali 36 zilizokuwepo katika Gaza, ni hospitali 19 tu ndizo ambazo bado zinafanya kazi kwa kiwango kidogo na kwa huduma chache mno.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha