Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (a.s.) - ABNA - maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametangaza kuwa waasi wanaohusishwa na ISIS wamewaua watu 66 mashariki mwa nchi hiyo.
Maafisa wa eneo hilo nchini Kongo wamewatambua waasi wa "Vikosi vya Kidemokrasia Vilivyoungana" (ADF), wanaohusishwa na ISIS, kuwa ndio waliohusika na shambulio dhidi ya raia katika eneo la Irumu na kuwaua.
Marcel Paluku, afisa wa eneo hilo huko Irumu karibu na mpaka wa Uganda, ameeleza kuwa wahanga waliuawa kwa mapanga na visu, na wanawake pia walikuwa miongoni mwa waliokufa.
Pia, idadi kadhaa ya watu wametekwa nyara, ingawa maelezo kuhusu idadi yao hayajatolewa.
Jean-Toby Okala, msemaja wa ofisi ya Umoja wa Mataifa mashariki mwa Kongo, ameelezea mauaji haya ya raia kama "umwagaji damu."
Vikosi vya Kidemokrasia Vilivyoungana (ADF) ni kundi la Uganda ambalo limepanua mashambulizi yake hadi mashariki mwa Kongo.
Idadi kamili ya wapiganaji wa ADF haijulikani. Kundi hili mara kwa mara huwashambulia raia.
Your Comment