15 Julai 2025 - 10:40
Source: ABNA
Wafanyakazi wa Bandari nchini Ugiriki Wazuiya Usafirishaji wa Bidhaa Kuelekea Utawala wa Kizayuni

Wafanyakazi wa bandari ya Piraeus nchini Ugiriki Jumatatu walizuia upakuaji wa shehena ya chuma cha kijeshi iliyokuwa ikielekea maeneo yanayokaliwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (ABNA), wafanyakazi wa bandari ya Piraeus nchini Ugiriki Jumatatu walizuia upakuaji wa shehena ya chuma cha kijeshi iliyokuwa ikielekea maeneo yanayokaliwa.

Katika mkutano uliofanyika katika gati namba 2 na 3 za bandari hiyo, wanachama wa chama cha wafanyakazi, waliojiunga na wanaharakati wanaounga mkono Palestina, makundi ya mrengo wa kushoto, na wabunge wa Chama cha Kikomunisti cha Ugiriki (KKE), walitangaza kwamba hawatakubali bandari hiyo kugeuka kuwa kituo cha kusaidia mauaji ya halaiki ya Wapalestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni.

Markos Bekris, Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari nchini Ugiriki, alisema: "Hatutaruhusu bandari hii kuwa kituo cha Marekani, NATO au Umoja wa Ulaya. Lengo letu ni kuzuia upakuaji wa shehena hiyo na kuzuia usafirishaji wa shehena hii hatari kwenda Israel. Hatutachafua mikono yetu kwa damu, hatutakuwa washirika na wakati huo huo hatutakuwa shabaha ya kulipizwa kisasi."

Your Comment

You are replying to: .
captcha