17 Julai 2025 - 11:27
Source: ABNA
Maandamano ya Watu wa Syria Yakikemea Mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni Dhidi ya Damascus

Watu kutoka maeneo mbalimbali nchini Syria walifanya maandamano Jumatano jioni katika maeneo mbalimbali nchini humo, wakikemea mashambulizi na uvamizi wa leo wa utawala haramu dhidi ya Damascus.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la AhlulBayt (ABNA), maandamano ya waandamanaji wa Syria kupinga uvamizi wa anga wa utawala haramu dhidi ya Damascus yamefanyika katika mikoa mbalimbali nchini humo, ikiwemo Aleppo, Latakia, Hama, na Damascus.

Katika maandamano yao, watu wa Syria walikemea vikali mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya makao makuu ya Amri Kuu ya Jeshi la Syria na Ikulu ya Rais, na kupiga nara dhidi ya utawala huo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetoa taarifa ikitangaza kuwa "Tunalaani vikali uvamizi wa kikatili wa Israel uliolenga taasisi za serikali na vituo vya kiraia leo huko Damascus - mji mkuu - na jimbo la Suwayda."

Wizara iliyotajwa ilisisitiza kwamba shambulio hili la wazi linafanyika ndani ya mfumo wa sera iliyolengwa ya utawala wa Israel ya kuchochea mvutano, kuunda machafuko, na kudhoofisha usalama na utulivu wa Syria.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesisitiza kuwa inahifadhi haki zake zote halali za kutetea ardhi na watu wake kwa njia zote zinazohakikishwa na sheria za kimataifa.

Your Comment

You are replying to: .
captcha