23 Julai 2025 - 17:28
Video | Helikopta ya Iran yakimbiza meli ya kivita ya Marekani kutoka kwenye Maji ya Iran

Asubuhi ya leo, helikopta ya Jeshi la Wanamaji iliisindikiza meli kuharibifu ya Kimarekani kutoka karibu na maji ya Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) -ABNA-, Asubuhi ya leo, Jumatano, Julai 23, 2025, mwendo wa saa 10:00 Asubuhi, meli ya kiuharibifu ya Kimarekani iitwaye DDG Fitzgerald ilikusudia kukaribia maji chini ya usimamizi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kulingana na ripoti hiyo, helikopta ya Jeshi la Wanamaji ya Iran iliruka haraka juu ya meli hiyo na kutoa onyo kali la kuondoka eneo hilo.

Katika kujibu, meli hiyo ya kiuangamizi na uharibifu ya Marekani ilitishia kulenga helikopta ya Iran na kuitaka iondoke eneo hilo. Hata hivyo, rubani wa Iran aliendelea na kazi yake kwa uthabiti na kwa mara nyingine tena akarudia onyo la kukaa mbali na maji ya Iran.

Katika kukabiliana na tishio hilo lililozushwa upya na meli hiyo ya Marekani, Mfumo wa Ulinzi wa ushujaa wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulichukua hatua na kutoa ujumbe thabiti kwamba helikopta hiyo ya majini iko chini ya uungaji mkono kamili wa mfumo wa ulinzi wa Iran na kwamba meli ya Marekani inatakiwa kubadili mkondo wake kuelekea kusini haraka iwezekanavyo.

Kwa msisitizo wa timu ya ndege na uungwaji mkono wa mfumo wa kiulinzi wa jeshi la Iran, meli mwangamizi ya Kimarekani iliyo na vifaa vya kijeshi, hatimaye ilijisalimisha na kuondoka kwenye maji ya Iran chini ya usimamizi wa Helkopta ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Video | Helikopta ya Iran yakimbiza meli ya kivita ya Marekani kutoka kwenye Maji ya Iran

Your Comment

You are replying to: .
captcha