Mwakilishi wa Iran huko UN alieleza haya jana huko New York baada ya kikao cha Baraza la Usalama kilichoitishwa kujadili pendekezo la Troika ya Ulaya dhidi ya Iran.
Mapema siku ya Alkhamisi Troika ya Ulaya inayoundwa na Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kwa jina na E3 iliwasilkisha rasmi taarifa katika Baraza la Usalama la UN ikitaka kuanza kutekelezwa mchakato kurejesha vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Iran (snapback). Vikwazo hivyo viliondolewa chini ya azimio nambari 2231.
Iravani ameongeza kuwa: "Iran imejitolea kufuata njia ya diplomasia, lakini kamwe haitafanya mazungumzo chini ya vitisho au kwa kulazimishwa. Amesema, hatua ya Troika ya Ulaya imechukuliwa kwa shabaha ya kuitisha Iran na kuiwekea mashinikizo ya kisiasa. Vilevile amesema nchi za Ulaya zinalitumia Baraza la Usalama la UN kama chombo cha kutimiza malengo yao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Iran kwa upande wake inasisitiza kuwa imejitolea kwa diplomasia, lakini haitafanya mazungumzo chini ya vitisho au kulazimishwa. Vilevile inaamini kuwa azimio nambari 2231 linapasa kutekelezwa kwa mujibu wa vipengee vyake asilia bila ya hila za kisiasa.
Mwakilishi na Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa nchi hii inasisitiza haki yake ya kuzalisha nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani na kwamba Baraza la Usalama halipasi kuruhusu kutumiwa vibaya na pande zilizokiuka azimio nambari 2231 na makubaliano ya JCPOA.
Your Comment