31 Agosti 2025 - 08:43
Source: Parstoday
Pezeshkian: Iran iko tayari kutumia misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi na kutoa mkono wa pole kwa serikali ya wananchi wa Pakistan kufuatia mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu wengi na kuharibiwa mali. Amesema Iran iko tayari kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko nchini Pakistan.

Rais Pezeshkian amezungumza kwa simu na Shehbaz Sharif, Waziri Mkuu wa Pakistan na kutilia mkazo uhusiano wa kihistoria na kindugu wa nchi mbili hizo. 

Katika mazungumzo hayo ya simu na Waziri Mkuu wa Pakistan, Rais wa Iran ameshukuru ukarimu na mazungumzo chanya aliyofanya na viongozi wa Pakistan wakati wa ziara yake ya hivi karibuni huko Islamabad.

Naye waziri Mkuu wa Pakikstan amemshukuru Rais Pezeshkian kwa salamu za rambirambi na mshikamano ulionyeshwa na wananchi wa Iran kwa wenzao wa Pakistan. Shehbaz Sharif amesema Iran na Pakistan siku zote zimekuwa bega kwa bega katika nyakati ngumu na kwamba nchi mbili zitaendelea kufanya hivyo. 

Iran na Pakistan zilikubaliana kufanya mkutano wa ana kwa ana pambizoni ya mkutano ujao wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko China ili kupitia upya mchakato wa ushirikino wa pande mbili na kimataifa. 

Mvua za masika zinazoendelea kunyesha huko Punjab, jimbo lenye wakazi wengi zaidi nchini Pakistan na hatua ya India ya kufungua maji mengi katika mabwawa yake kuelekea nchi jirani ya Pakistan baada ya kujaa pakubwa kwa maji vimesababisha mafuriko ambayo hayajawahi kushuhudiwa katikati mwa Pakistan, na hadi sasa yamesababisha hasara kubwa ya kifedha na kugharimu maisha watu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha