3 Septemba 2025 - 00:14
Source: Parstoday
Pendekezo la Iran kwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai; hatua ya kuelekea kwenye mfumo mpya wa dunia

Katika hotuba yake katika kikao cha Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, Rais Masoud Pezeshkian wa Iran aliwasilisha utatuzi uliopendekezwa na Iran kwa ajili ya kupanua ushirikiano kati ya wanachama wa jumuiya hiyo kwa lengo la kukabiliana na misimamo ya upande mmoja ya Marekani na Magharibi.

Pezeshkian, ambaye aliwasili juzi katika mji wa Tianjin nchini China, jana Jumatatu alihuhutubia Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) na kusisitiza nafasi muhimu ya jumuiya hiyo katika kuandaa muundo wa dunia ya kambi kadhaa na kuzitaka nchi wanachama kufuatilia mikakati ya pande nyingi ya kuimarisha amani na ushirikiano wa kifedha duniani. 

Ili kukabiliana na athari za vikwazo vya upande mmoja, Rais Pezeshkian amezindua akaunti maalumu ya jumuiya ya SCO na utaratibu wa kutatua masuala mbalimbali.

Rais wa Iran amesema kuwa ubunifu huu unalenga kupunguza utegemezi kwa dola ya Marekani.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais wa Iran amelaani mashambulizi ya hivi karibuni ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, pamoja na vita na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza, na kusema haya yote yanadhihirisha kushindwa kikamilifu kwa mfumo wa sasa wa uongozi wa dunia.

Rais Masoud Pezeshkian ameunga mkono pia mapendekezo ya kuanzishwa vituo maalumu vya kupambana na vitisho vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na biashara ya madawa ya kulevya na ugaidi.

Rais wa Iran amesisitiza kuwa: Iran, kwa kuegemea nafasi yake ya kipekee ya kijiografia na kisiasa, imejiandaa pia kutoa jukwaa linalohitajika kwa ajili ya kupanua ushirikiano wa kieneo na kuunda fursa za kufikia mataifa mengine.

Pendekezo la Iran kwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai; hatua ya kuelekea kwenye mfumo mpya wa dunia

Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) katika mkutano wa China

Umuhimu wa ushirikiano wa Iran na wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) unaweza kuchunguzwa katika nyanja tatu kuu: uchumi, siasa na usalama. Ushirikiano huu sio tu kwamba unaimarisha nafasi ya kieneo ya Iran, bali pia unatoa fursa za kistratijia za maingiliano na madola yanayoibukia duniani.

Uanachama katika Jumuiya yaShirika la Ushirikiano ya Shanghai (SCO) unaruhusu maingiliano ya kiuchumi na nchi kama vile China, India, na Russia, ambazo kwa pamoja zinachukua zaidi ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni. Iran inaweza kushiriki katika miradi mikubwa na kunufaika na uwekezaji katika uchukuzi, nishati na teknolojia.

Ushirikiano na nchi za Mashariki unaweza kusaidia kupunguza athari za vikwazo vya Magharibi na kuunda njia mbadala za mabadilishano ya kibiashara na kifedha.

Kushiriki kikamilifu katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai kunairuhusu Iran kuchukua nafasi katika kufanya maamuzi ya kikanda na kuwasilisha maoni yake katika vikao vya kimataifa. Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai inatoa jukwaa la ushirikiano wa kiitelijensia na usalama katika kupambana na vitisho vya kawaida kama vile ugaidi, ulanguzi wa dawa za kulevya na uhalifu uliopangwa.

Pendekezo la Iran kwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai; hatua ya kuelekea kwenye mfumo mpya wa dunia

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian akihutubia mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai uliofanyika nchini China

Ushirikiano wa kiusalama wa Iran na nchi jirani na madola ya kikanda unaweza kusaidia kupunguza mivutano na kuongeza utulivu katika Asia Magharibi na Asia ya Kati.

Sifa za kipekee za kiuchumi na kijiografia za Iran zimeunda mazingira mazuri ya kupanua ushirikiano wa kina na wanachama wengine wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Eneo la kijiografia la Iran ikiwa njia panda ya Mashariki-Magharibi na Kaskazini-Kusini kumeifanya kuwa mshirika mkuu katika miradi ya uchukuzi na usafiri wa kikanda.

Pendekezo la Rais Masoud Pezeshkian katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai lina umuhimu wa kistratijia kwa njia kadhaa na linaweza kuwa na nafasi katika kukabiliana na vikwazo vya upande mmoja vya Magharibi. Iran imetilia mkazo nafasi ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai kama moja ya nguzo za kuunda pande nyingi duniani na kusema kuwa, ushirikiano kati ya nchi wanachama satwa na uchuukuaji maamuzi wa upande mmoja wa nchi za Magharibi na kusaidia kuleta uwiano katika uhusiano wa kimataifa.

Pendekezo hili sio tu ni jibu kwa vikwazo, lakini ni jaribio la kufafanua upya nidhamu ya kimataifa kupitia ushirikiano huruu wa kikanda na kifedha. Iwapo hili litatekelezwa, linaweza kupunguza athari za vikwazo vya Magharibi na kuzifanya nchi wanachama kusimama kidete mbele ya mashinikizo ya kiuchumi na kisiasa.

Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai unaweza kuwa mwanzo kwa nchi huru kukusanyika pamoja ili kupitisha utendaji muhimu wa kisiasa, kiuchumi na kiusalama ili kukabiliana na tamaa na upendaji makuu wa Marekani na nchi za Magharibi, mtazamo ambao daima umekuwa sehemu muhimu ya sera za kigeni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Your Comment

You are replying to: .
captcha