Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu Al Jazeera, vyanzo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa kamati imeundwa na Wizara za Vita na Fedha za utawala huo ili kuboresha mchakato wa matibabu ya wanajeshi wa Kizayuni waliojeruhiwa.
Hatua hii ya wizara hizo inafuatia ongezeko la idadi ya wanajeshi waliojeruhiwa katika vita vya Gaza.
Pia, gazeti la Yedioth Ahronoth, likinukuu idara ya ukarabati ya Wizara ya Vita ya utawala wa Kizayuni, liliripoti kwamba idadi ya wanajeshi waliojeruhiwa wanaotibiwa itafikia 100,000 kufikia mwaka 2028.
Inafaa kuashiria kwamba miaka miwili baada ya kuanza kwa vita vya Gaza, vikosi vya upinzani vya Palestina bado vinaendelea na operesheni zao za kupinga Uzayuni katika maeneo mbalimbali ya Ukanda huo.
Your Comment