Rais Pezeshkian leo alielekea Doha kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa viongozi wa Kiislamu na Kiarabu wenye lengo la kujadili mashambulio ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Qatar.
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akizungumza mapema leo kabla ya kuelekea Qatar alisisitiza kuwa, nchi za Kiislamu lazima ziongeze umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Pezeshkian amesema: "Nchi za Kiislamu zinapaswa kushikamana na kukata uhusiano wao na utawala wa Kizayuni kwa kuchukua hatua za kivitendo katika nyanja za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii."
Masoud Pezeshkian amesema: "Kikao hiki kinafanyika kwa mwaliko wa Amir wa Qatar na kitashughulikia suala la hujuma ya wazi ya utawala wa Kizayuni iliyofanyika dhidi ya Qatar licha ya sheria zote za kimataifa."
Huku akisisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni hautambui fremu yoyote unaojiwekea yeye mwenyewe, ameongeza kuwa: "Utawala huu umezishambulia nchi nyingi za Kiislamu zikiwemo Qatar, Lebanon, Iraq, Iran na Yemen. Unafanya chochote utakacho, na kwa bahati mbaya, Marekani na nchi za Ulaya nazo zinaunga mkono hatua hizo."
Rais wa Iran ameongeza kuwa: "Utawala huu unafanya mauaji ya halaiki huko Gaza, unawahukumu kifo wanawake, watoto na wazee, na kwa bahati mbaya, madaola yanayopiuunga mkono utawala huu ghasibu yanahalalisha vitendo hivi kwa uungaji mkono na misaada yao kwa utawala wa kibaguzi wa Kizayuni."
Amesisitiza kuwa: "Iwapo Waislamu watashikamana, maadui hawatathubutu kuzivamia nchi zetu na kukiuka sheria zote za kimataifa."
Your Comment