4 Oktoba 2025 - 22:42
Kwa nini Wahaabi wanakataa Hadithi za kuwasilishwa kwa matendo yetu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)?

Qur’ani Tukufu imebainisha wazi katika Aya kadhaa kwamba Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na hata Waumini (ambao kwa mujibu wa riwaya za Kishia, ni Maimamu watoharifu -Ahlul-Bayt (a.s)- wana habari kuhusu matendo ya watu. Uwasilishaji huu wa matendo hutokea duniani na Akhera.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Moja ya hoja madhubuti zinazoonyesha batili ya itikadi za Wahaabi ni ile elimu tukufu ya kwamba matendo ya wanadamu huwasilishwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Hata hivyo, Wahaabi wanadai kwamba ikiwa Mtume amefariki dunia, vipi basi matendo ya watu yanaweza kuwasilishwa kwake?.

Lakini Qur’ani Tukufu imebainisha wazi katika Aya kadhaa kwamba Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na hata Waumini (ambao kwa mujibu wa riwaya za Kishia, ni Maimamu watoharifu -Ahlul-Bayt (a.s)- wana habari kuhusu matendo ya watu. Uwasilishaji huu wa matendo hutokea duniani na Akhera.

Riwaya sahihi kutoka madhihaba ya Shia na Sunni zinathibitisha kuwa matendo ya wanadamu huwasilishwa kwa Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu watoharifu (a.s.), na jambo hili huleta furaha au huzuni kwao kulingana na matendo yetu.

Elimu hii tukufu haipingani na ujuzi wa Mwenyezi Mungu, bali humhimiza Mwislamu kuwa mwangalifu katika mwenendo na matendo yake, na kuendelea kujilea kiroho na kimaadili kwa kutambua kuwa matendo yake yako wazi mbele ya Mtume na Ahlul-Bayt (a.s).

Your Comment

You are replying to: .
captcha