24 Novemba 2025 - 21:51
Source: ABNA
Majibu ya “Al-Qassam” Kufuatia Shahada ya Kamanda Mashuhuri wa Hizbullah

Brigedi za Izz ad-Din al-Qassam zimetoa majibu kwa shahada ya kamanda mashuhuri wa Hizbullah katika shambulio la kihalifu la utawala wa Israel dhidi ya Dahiya Kusini mwa Beirut.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la ABNA likinukuu shirika la habari la Palestina la Shahab, Brigedi za Shahidi Izz ad-Din al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Hamas, zilitangaza katika taarifa: Kwa heshima kubwa, utukufu, na imani katika ahadi ya ushindi wa Mwenyezi Mungu, tunatoa pole kwa shahada ya kamanda mashuhuri wa muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon, Shahidi Haitham Ali Tabatabaei, kiongozi wa amri ya kijeshi ya muqawama wa Kiislamu.

Taarifa hiyo inasema: Kamanda shahidi "Sayyid Abu Ali" aliuawa shahidi katika njia ya kutetea Quds pamoja na kundi la ndugu zake mujahidina, katika shambulio la kihalifu la utawala wa Kizayuni dhidi ya Dahiya Kusini mwa Beirut.

Brigedi za Qassam ziliendelea kusifu jukumu la shahidi huyu mkuu katika kuunga mkono watu wa Palestina na muqawama wao wakati wa vita vya "Kimbunga cha Al-Aqsa" na kusisitiza kwamba Shahidi Tabatabaei alikuwa na jukumu muhimu katika kuunda na kuimarisha uwanja wa muqawama dhidi ya wakaliaji kimabavu wa Kizayuni katika miaka mingi ya mapambano.

Utawala wa Kizayuni ulishambulia Dahiya Kusini mwa Beirut kwa shambulio la anga Jumapili alasiri (2 Azar kulingana na kalenda ya Iran), ambapo angalau watu 5, akiwemo Haitham Abu Ali Tabatabaei, kamanda mashuhuri wa Hizbullah ya Lebanon, waliuawa shahidi na idadi kadhaa walijeruhiwa.

Your Comment

You are replying to: .
captcha