17 Desemba 2025 - 13:27
Source: ABNA
Harakati za Israel nchini Yemen kupitia mamluki wa Imarati (UAE)

Mwanaharakati wa kisiasa wa Yemen ameonya dhidi ya harakati za utawala wa Kizayuni nchini humo kupitia mkono wake wa Imarati ili kufikia maslahi yake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu Al-Maalouma, Aref Muthanna al-Amiri, mwanaharakati wa kusini mwa Yemen, alisema kuwa matukio yanayoendelea nchini humo ni sehemu ya mradi wa kikanda na kimataifa wa kupanga upya maeneo ya ushawishi wa pande za kigeni. Alisisitiza kuwa uwepo wa Imarati nchini Yemen hauwezi kutenganishwa na mipango ya Israel. Israel inawaunga mkono wanachama wa Baraza la Mpito la Kusini (mamluki wa Imarati) ili kuidhoofisha Yemen.

Al-Amiri alibainisha kuwa kufeli kwa Imarati kumepelekea Marekani na Israel kuingilia kati ili kulazimisha mazingira mapya. Katika siku za hivi karibuni, maeneo ya mashariki na kusini mwa Yemen yameshuhudia mapigano kati ya mamluki wa Saudi Arabia na wale wa Imarati. Wakati Riyadh ikianza kusajili vikosi mkoani Al-Mahra kupambana na mamluki wa Imarati, vikosi vinavyoungwa mkono na Imarati vimetangaza kusitisha ushirikiano na serikali inayoungwa mkono na Riyadh.

Your Comment

You are replying to: .
captcha