17 Desemba 2025 - 13:30
Source: ABNA
Mmoja wa viongozi hatari zaidi wa Daesh anaswa na vikosi vya Iraq

Vikosi vya usalama nchini Iraq vimefanikiwa kumtambua na kumkamata mmoja wa viongozi hatari zaidi wa Daesh baada ya operesheni kubwa ya ufuatiliaji.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu Al-Maalouma, kukamatwa huku kumekuja baada ya operesheni ya miezi kumi ya kufuatilia mienendo ya kiongozi huyo. Ripoti hiyo inasema kiongozi huyo alifuatiliwa na kukamatwa mara tu aliporejea nchini Iraq akitokea katika nchi moja jirani.

Kiongozi huyo, anayejulikana kwa jina la Abu Alia, anachukuliwa kuwa mmoja wa wanachama hatari zaidi wa kundi hilo. Alianza harakati zake tangu mwaka 2004 mjini Baghdad, akibobea katika kutengeneza mabomu. Uchunguzi unaonesha kuwa alihusika moja kwa moja katika mashambulizi ya kigaidi maeneo mbalimbali ya Baghdad. Wakati wa operesheni za kusafisha Iraq, alikimbilia mikoa ya Salahuddin na Kirkuk kabla ya kutorokea nje ya nchi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha