Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA likinukuu Al Jazeera, tukio hilo lilitokea katika mtaa wa Al-Daraj katikati ya mji wa Gaza, ambapo mtu mwingine mmoja alijeruhiwa. Tukio hili limetokea huku mzingiro wa utawala wa Israel dhidi ya Gaza ukiendelea na kuzuia kuingia kwa misaada ya kutosha.
Katika tukio jingine, binti mdogo kwa jina Malak Rami Ghneim alifariki dunia kutokana na baridi kali katika kambi ya Nuseirat. Matukio haya yanatokea katika mazingira magumu sana ya kibinadamu ambapo mamia ya maelfu ya Wapalestina wanaishi katika mahema yasiyo na vifaa vya usalama. Ukosefu wa umeme na mafuta unawalazimu kutumia njia duni za kupasha joto, jambo ambalo huongeza hatari ya moto.
Your Comment