Kwa mujibu wa ABBA ikinukuu Al Jazeera, jeshi la serikali ya Kizayuni lilikiri kwamba tangu kuanza kwa makubaliano ya kusitisha mapigano hadi sasa, jeshi la anga la serikali hiyo limelenga zaidi ya pointi 1100 nchini Lebanon.
Jeshi la uvamizi la Israel lilidai kwamba pointi hizi zilikuwa ni za miundo mbinu ya Hizbullah. Hali halisi, kulingana na ripoti rasmi zilizochapishwa nchini Lebanon, mashambulizi ya serikali ya Kizayuni yamelenga pia vituo vya afya, magari ya wagonjwa, wanahabari na wafanyakazi wa matibabu.
Wizara ya Afya ya Lebanon Jumatatu ilitangaza kwamba idadi ya mashahidi wa nchi hiyo kutokana na mashambulizi ya serikali ya Kizayuni tangu Machi 2 mwaka huu imeongezeka hadi 2869.
Hali kadhalika, tangu tarehe hiyo hadi sasa watu 8730 pia wamejeruhiwa.
Jeshi la serikali ya Kizayuni lilikiri kufanya mamia ya mashambulio dhidi ya Lebanon katika kipindi cha kile kinachoitwa kusitisha mapigano.
Your Comment