Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, ametoa kauli kufuatia kile alichokitaja kuwa ni kauli kinzani zinazotolewa na baadhi ya maafisa wa Serikali ya Marekani kuhusu mazungumzo ya kidiplomasia yanayoendelea.
Baghaei amesema kuwa ni jambo la kawaida katika mchakato wowote wa mazungumzo ya kidiplomasia kwa kila upande kujaribu kuwasilisha simulizi lake, hata hivyo Iran imejitahidi kuhakikisha kuwa simulizi lake linatokana na uhalisia na linaendana na ukweli.
Ameongeza kuwa Iran imekuwa ikitoa taarifa kwa uwazi kwa wananchi wake tangu mwanzo wa mchakato wa mazungumzo yanayohusisha upatanishi wa Pakistan, ambapo Tehran ilieleza wazi misimamo yake pamoja na masuala ambayo inayaona kuwa ya msingi na “mipaka isiyoweza kuvukwa” katika mazungumzo hayo.
Baghaei alisisitiza kuwa Iran itaendelea kushikilia misimamo yake ya msingi huku ikijitahidi kuendeleza mazungumzo kwa misingi ya uwazi, heshima na ukweli.
13 Juni 2026 - 16:02
News ID: 1826289
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, amesema kuwa katika mchakato wowote wa kidiplomasia kila upande hujaribu kuwasilisha simulizi lake, lakini Iran imekuwa ikihakikisha taarifa zake zinatokana na uhalisia na uwazi kwa wananchi.
Your Comment