6 Julai 2026 - 22:36
Mkuu wa Mhimili wa Mahakama Awashukuru Waombolezaji wa Mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei

Mkuu wa Mhimili wa Mahakama wa Iran amesema mahudhurio ya mamilioni ya wananchi katika mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei yameandika ukurasa mpya wa historia ya mshikamano, heshima na uimara wa taifa la Iran.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mkuu wa Mhimili wa Mahakama wa Gholam-Hossein Mohseni-Ejei ametoa ujumbe wa shukrani kwa wananchi wa Iran kufuatia ushiriki wao wa mamilioni katika hafla ya kuaga na mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

Katika ujumbe wake uliotolewa Jumatatu, Mohseni-Ejei alisema kuwa wananchi wa Iran wameandika ukurasa mpya wa heshima, mshikamano na uzalendo kwa kujitokeza kwa wingi katika mazishi hayo, jambo ambalo, kwa mujibu wake, limewavunja moyo maadui na kuonyesha uimara wa taifa la Iran.

Alisema: "Enyi wananchi wakubwa na wa kushangaza wa Iran, mmeandika tena simulizi la nuru, heshima na ushujaa. Ninyi ni taifa lililobeba ujumbe mkubwa; leo mmeandika tukio la kihistoria lenye athari za kitaifa na kimataifa katika kurasa za historia."

Mkuu huyo wa Mahakama aliwatakia wananchi hao waendelee kuwa imara katika misingi yao na kudumisha bendera ya azma, uhuru na mshikamano ikiwa juu daima.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha