Kwa mujibu wa shirika la habari ABNA kwa kunukuu shirika la habari la Al Jazeera, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani leo Jumamosi ilitangaza katika taarifa: Wamarekani waliopo Mashariki ya Kati (Magharibi mwa Asia) wanapaswa kuwa waangalifu zaidi na kujiandaa kwa kufungwa kwa anga na usumbufu unaoweza kutokea katika safari.
Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuhusu hili imesema: Wamarekani waliopo katika eneo hilo wanapaswa kuzingatia kuondoka au kujiandaa kuondoka katika eneo hilo iwapo mvutano utazidi kuongezeka. Wamarekani walio nje ya Mashariki ya Kati (Magharibi mwa Asia) wanapaswa kufikiria upya kuhusu kusafiri katika eneo hili.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliongeza: Iran na makundi yanayohusiana nayo yanaweza kulenga maslahi ya Marekani duniani kote!
Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad hapo awali ulikuwa umewaonya raia wa Marekani kuhusu kuongezeka kwa mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati (Magharibi mwa Asia).
Ubalozi wa Marekani nchini Iraq uliwaonya raia wa Marekani kuwa waangalifu sana, kuongeza kiwango cha uangalifu wao, na kujiandaa na uwezekano wa kughairiwa kwa safari za ndege, kufungwa kwa muda kwa anga, na usumbufu katika usafiri.
Maoni yako