Mapigano makali yanaendelea mjini Mogadishu Somalia na kwa akali wanajeshi 16 wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika AMISOM wameuawa katika mapigano baina yao na wanamgambo wa as Shabab. Mapigano hayo ambayo yalizuka katika kitongoji kimoja mjini Mogadishu wakati vikosi vya Umoja wa Afrika vilivyopokuwa vikijaribu kuwafurusha wanamgambo wa as Shabab kutoka katika ngome yao hiyo yamesababisha wasi wasi mkubwa.Wakati huo huo wanagambo wa ash Shabab wamedai kwamba wamewaua wanajeshi 70 wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika. Wakati huo huo, Felix Kulaigye Msemaji wa Jeshi la Uganda amesema kuwa, miili ya wanajeshi 6 wa nchi hiyo waliuawa huko Somalia juma lililopita imewasili nchini humo na kukabidhiwa kwa familia zao kwa ajili ya taratibu za mazishi. Hayo yanajiri katika hali ambayo vikosi vya Kenya vimeingia katika ardhi ya Somalia kwa shabaha ya kupambana na wanamgambo wa ash Shabab ambao wamekuwa wakihatarisha usalama katika mpaka wa Somalia na Kenya
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 273676
Mapigano makali yanaendelea mjini Mogadishu Somalia na kwa akali wanajeshi 16 wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika AMISOM wameuawa katika mapigano baina yao na wanamgambo wa as Shabab