Shirika la habari la Xinhua limemnukuu Mkuu wa Jeshi la Syria, Jenerali Fahd Jassem al-Freij akisema kwamba serikali ya nchi hiyo imeimarika zaidi hivi sasa kufuatia mgogoro wa miezi ya hivi karibuni na bado imeendelea kushikamana na misingi yake ya kitaifa.Al-Freij ameongeza kuwa, nchi za Magharibi na hasa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinafanya njama za kuvuruga mshikamano wa wananchi wa Syria na kuidhoofisha nchi hiyo kutokana na misimamo yake ya kupinga Israel na ubeberu wa nchi za Ulaya na kutokubali kuburuzwa.Mkuu huyo wa jeshi la Syria amesisitiza kuwa, wananchi wa nchi hiyo wanapinga uingiliaji wa aina yoyote ile wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya nchi yao na wanaunga mkono juhudi za marekebisho ya kisiasa zinazoendelea kufanywa na Rais Bashar al Assad.Aidha amevilalamikia vyombo vya habari vinavyoendesha propaganda mbaya dhidi ya Syria na kuhoji akisema, kwa nini vyombo hivyo vinanyamazia kimya uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu unaofanywa na Israel huko Palestina na kusini mwa Lebanon lakini wakati huo huo vinakuza kupindukia mambo ya ndani ya Syria?
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 273875
Afisa mmoja wa kijeshi nchini Syria amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo imeimarika zaidi baada ya machafuko ya hivi karibuni nchini humo.