Beatrice Kisaro, Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo ya kieneo amesema kuwa, ugaidi unaotekelezwa na kundi hilo lililofurutu ada la Somalia usipodhibitiwa, basi huenda ukawa na taathira hasi katika maendeleo, ushirikiano na uhusiano kati ya nchi wananchama wa EAC. Kisaro amesema hayo alipokuwa akizungumza katika warsha ya siku mbili iliyoanza jana mjini Arusha Tanzania kuhusu namna ya kubuni ramani ya njia ya kuanza kufanya kazi "Utaratibu wa Tahadhari ya Mapema" katika Afrika Mashariki.Siku ya Jumatatu, kulitokea mashambulio mawili ya maguruneti kwa nyakati tofauti jijini Nairobi na kusababisha mauaji ya mtu mmoja na makumi ya wengine kujeruhiwa. Kundi la Al Shabaab limetishia kuwa litaishambulia Kenya kwa kutuma vikosi vyake nchini Somalia. Vikosi hivyo vya Kenya tayari vimekwishateka miji kadhaa ya Somalia na sasa vinafanya jitihada za kuteka mji wa kiistratejia wa Kismayu, ngome muhimu ya al Shabaab.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 274397
Jumuiya ya Afika Mashariki imelaani mashambulio ya kigaidi yanayotekelezwa na kundi la wanamgambo wa al Shabaab la Somalia nchini Kenya.