19 Machi 2011 - 20:30

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Wamagharibi walituma vikosi vyao vya NATO nchini Libya sio kwa lengo jingine ghairi ya kutafuta njia ya kunyonya utajiri na maliasili ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Wamagharibi walituma vikosi vyao vya NATO nchini Libya sio kwa lengo jingine ghairi ya kutafuta njia ya kunyonya utajiri na maliasili ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.Akizungumza leo katika mkoa wa Khorasan Kusini ulioko mashariki mwa Iran, Rais Mahmoud Ahmadinejad amewataka wananchi wa Libya wawe macho kutokana na njama za Wamagharibi za kutaka kuteka ushindi wa harakati zao za kimapinduzi. Rais Ahmadinejad amesema kuwa, leo madola ya kibeberu yanafanya juu chini ili kupanua satua na ushawishi wao na yanatumia njia za propaganda za kisiasa na kuweka kambi za kijeshi katika nchi nyingine kwa kisingizio cha kulinda maslahi, uhuru na haki za wananchi.Rais wa Iran ameongeza kuwa, zama za udikteta, dhulma na uingiliaji katika masuala ya ndani ya nchi nyingine zimepitwa na wakati kutokana na kuamka wananchi si tu wa eneo hili la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika bali wa ulimwenguni kote.