19 Machi 2011 - 20:30

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya inayoshughulikia misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Somalia imesema taifa hilo la Pembe ya Afrika bado linapitia kipindi kigumu cha njaa iliyoyakumba maeneo mengi ya nchi hiyo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya inayoshughulikia misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Somalia imesema taifa hilo la Pembe ya Afrika bado linapitia kipindi kigumu cha njaa iliyoyakumba maeneo mengi ya nchi hiyo. Taarifa ya ofisi hiyo imesema kuwa, hivi sasa Somalia inakabiliwa na matatizo makubwa yaliyosababishwa na vita na njaa, ikiwa ni pamoja na wimbi kubwa la wakimbizi wa ndani wanaomiminika mjini Mogadishu, jambo ambalo linasababisha ugumu wa kuwahudumia na kuwasaidia watu hao.Taarifa hiyo ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya inayoshughulikia misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Somalia imeongeza kuwa, hivi sasa ofisi hiyo inafanya juu chini lulusanya misaada zaidi itakayoweza kukidhi mahitaji ya mamilioni ya watu hususan chakula katika maeneo yote yaliyoathirika. Kundi la al Shabaab ambalo linaendelea kukabiliwa na mashambulizi ya vikosi vya jeshi la Kenya na serikali ya mpito ya nchi hiyo limekuwa likizuia misaada ya kibinadamu kuwafikia mamilioni ya raia wanaosumbiliwa na njaa nchini humo.