Abdulrahman Shalgham Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Libya ambaye pia ni mwakilishi wa sasa wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa amewatuhumu viongozi wa serikali ya Qatar kuwa wana lengo la kuidhibiti Libya. Shalgham amesisitiza pia kwamba Libya haitakuwa nchi yenye mfungamano na Qatar. Amesema, viongozi wa Qatar wamewasilisha matakwa yao wakati walipokutana na ujumbe wa Baraza la Mpito la Libya, matakwa ambayo yametajwa na mjumbe huyo wa Libya katika Umoja wa Mataifa kuwa yasiyokubalika. Abdulrahman Shalgham amekataa pia kupewa Qatar mamlaka ya kuongoza wanajeshi wa kimataifa walioko nchini humo na kuituhumu Doha kuwa haitekelezi uadilifu katika kuamiliana na makundi mbalimbali huko Libya.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 276505
Mwakilishi wa Libya katika Umoja wa Mataifa amewatuhumu viongozi wa Qatar kuwa wanaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo