Serikali ya Khartoum imetangaza kuwa serikali ya Juba inawasaidia waasi wa eneo la Blue Nile kwa kuwapa makombora ya anga, vifaru, mabomu na zana nyinginezo za kivita. Kuhusiana na suala hilo, Dafiullah al Haji Ali Othman mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa kuna nyaraka na ushahidi kuwa viongozi wa Sudan Kusini wanawaunga mkono waasi wa eneo la Kordofan Kusini na Blue Nile. Mikoa hiyo mawili iko katika mpaka wa Sudan na Sudan Kusini na kwa muda mrefu imekuwa kiunganishi cha waasi wa mikoa hiyo miwili na harakati ya Ukombozi wa Sudan, yaani mrengo unaotawala huko Sudan Kusini.Hivi sasa pia Harakati ya Ukombozi wa Sudan inawatumia waasi wa mikoa ya Kodrofan Kusini na wajimbo la Blue Nile kwa ajili ya kuishinikiza serikali ya al Bashir kwa kutumia misaada ya hali na mali inayotolewa na nchi za Magharibi na utawala wa Kizayuni kwa Sudan Kusini. Hayo yanajiri katika hali ambayo eneo la mpakani na lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Abyei huko katika mpaka wa pamoja wa Sudan na Sudan Kusini linaendelea kushuhudia mapigano na mikwaruzano ya mara kwa mara kati ya vikosi vya usalama vya nchi mbili hizo.Japokuwa kumefanyika mazungumzo kati ya Sudan na Sudan Kusini kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa matatizo kati ya pande hizo, lakini viongozi wa Sudan wanaamini kuwa, kuna baadhi ya pande zinazokwamisha mazungumzo hayo kwa lengo la kuanzisha vita vingine kati ya Khartoum na Juba. Serikali ya Khartoum imeutaja utawala ghasibu wa Israel kuwa inachochea moto mpya wa vita kati ya Sudan na Sudan Kusini. Khartoum imeuomba Umoja wa Mataifa usaidie na kuingilia kadhia hiyo iliyojitokeza sasa kati yake na Sudan Kusini na hata kuamua kuwasilisha malalamiko yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hii ni mara ya pili Khartoum inawasilisha malalamiko yake dhidi ya Sudan Kusini katika Baraza la Usalama tangu Juba itangaze uhuru wake mwezi Julai mwaka huu. Baadhi ya duru za kisiasa zinaona kuwa si jambo lililo mbali kutokea mikwaruzano mikubwa zaidi kati ya pande hizo mbili kwa kuzingatia vita vya maneno na vya kidiplomasia vinavyoendelea sasa kati ya Juba na Khartoum. Hii ni katika hali ambayo Khartoum imepinga suala hilo, lakini wakati huohuo imeeleza kuwa itatoa jibu kali kwa hatua yoyote ya serikali ya Juba ya kujaribu kuvuka mistari myekundu ya Sudan.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 277404
Rais Omar al Bashir wa Sudan ameionya nchi changa ya Sudan Kusini kuhusu mikwaruzano yoyote itakayoanzishwa na nchi hiyo, baada ya kuzuka mapigano kati ya wanajeshi wa Sudan na Sudan Kusini. Al Bashir amesema kuwa Khartoum haina azma ya kuanzisha vita, lakini iwapo Juba itaishambulia Sudan, basi nchi yake itatoa jibu kali na somo lisiloweza kusahaulika kwa Sudan Kusini. Rais wa Sudan pia ameelekeza kidole cha tuhuma kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na kueleza kuwa, Sudan Kusini imevuruga amani katika maeneo ya mpakani kwa kuchochewa na utawala huo.