Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Sheikh Sharif Ahmad wa Serikali ya Mpito ya Somalia wameyasema hayo katika mkutano wao mjini Nairobi hii leo. Viongozi hao wamesema wana imani kuwa oparesheni ya pamoja ya kijeshi ya Kenya na serikali ya Somalia ni fursa ya kihistoria ya kurejesha uthabiti na usalama Somalia. Baada ya mkutano wa marais hao wametoa taarifa ya pamoja iliyosomwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Moses Wetangula. Taarifa hiyo imesema viongozi hao walisisitiza haja ya ushirikiano baina ya vikosi vya Umoja wa Afrika Somalia, serikali ya mpito ya Somalia na Jeshi la Ulinzi la Kenya katika kuangamiza waasi wa al Shabab na makundi mengine yanayotishia amani katika eneo la Pembe na Afrika na dunia. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa nchi hizo tatu.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 278657
Marais wa Kenya, Uganda na Somali wametoa wito wa ushirikiano wa kieneo kurejesha utulivu Somalia.