Shirika la habari la Ahlul bayt linatuarifu kuwa :Majaji wa jiji la Toronto walipitisha mswada wa kuruhusu mabanati wa kiislamu kuvaa hijabu tangu miezi mitano iliyopita ama mswada huu kwa polisi wa kike umenza kufanya kazi rasmi hapo jana. vyombo vya habari vya Canada vinatuarifu kuwa, wakuu wapolisi wa nchi hiyo wamepitisha rasmi mswada huo na kuwa ruhusu mabanati ambao ni polisi kuhudhuria kazini na vazi hilo tukufu lenye kuleta heshima na taadhima kwa mabanati. Bwana Farnandus ambaye alikuwa ni Kamanda mkuu wa jeshi la polisi la Toronto anatuambia kuwa:Kamanda mpya wa polisi wa jiji hilo alipitisha mswada huo kwa polisi wa kike wa jiji hilo, baada ya kufanya kikao na viongozi wa kiislamu wa jiji hilo,hii imetokea baada ya kuonekana kuwa wengi wa waislamu wamekuwa wakijiuga na jeshi la polisi katika jiji hilo.Anaendelea kusema: idadi ya waumini wa dini ya kiislamu katika jiji la Toronto kila siku inaongezeka hivyo hatuna budi kuwatekelezea matakwa yao.Mona Tabesh ni afisa wa kike wa jeshi la polisi la jiji la Toronto ambaye ameonekana kuzingatia vazi la hijabu kwa kipindi kirefu, amekuwa ni mfano wa kuigwa mara tu baada ya kupitishwa mswada huo wa kuvaa hijabu kazini.Yafaa kuashiria kuwa Mona Tabesh na mwenendo wake wa kuzingatia vazi hilo la stara, anafaa kuwa ni somo tosha na mfano wa kuigwa na mabanati wengine wa kiislamu.Pia wakuu wa Idara za polisi wa Toronto wanaazma ya kupitisha mswada wa kufunguliwa migahawa na mabucha ya kiislamu yatakayo uza nyama halali kwa waumini wa kiislamu.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 279983
Idara ya Polisi ya Jiji la Toronto Canada imepitisha mswada wa kuruhusu kuvaa hijabu askari wake wa kiislamu wanaotumikia jeshi hilo.