19 Machi 2011 - 20:30

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Lebanon amesema kuwa,nchi yake inapinga kuwekewa vikwazo Syria.

Adnan Mansour sanjari na kulaani vikwazo dhidi ya Syria amesema, taifa la Lebanon na serikali ya Beirut haikubaliana na vikwazo vya aina yoyote ile dhidi ya serikali ya Damascus. Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Lebanon amesisitiza kwamba, vikwazo dhidi ya Syria vina matashi ya kisiasa hivyo nchi yake haiwezi kukubaliana navyo. Wakati huo huo, Nabih Berri Spika wa Bunge la Lebanon nae kwa upande wake ameashiria matukio ya Syria na kusema kwamba, kwa sasa Mashariki ya Kati inaandamwa na njama za kila upande hivyo ulimwengu wa Kiislamu na watu huru duniani hawana budi kuwa macho na njama hizo.