Ripoti ya hivi karibuni kabisa iliyotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu imesema kuwa, Wazayuni wanawabagua raia wenye asili ya Kiarabu wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu. Ripoti hiyo imesema kuwa, hali ya Waarabu waishio chini ya utawala wa Kizayuni nimbaya mno ikija katika mambo ya msingi kama vile elimu, makazi na ardhi.Ripoti hiyo yenye kurasa 27 imeongeza kuwa, inasikitisha kuona Waarabu wapatao milioni 1.37 ambao wanaunda asilimia 20 ya idadi jumla ya wakazi waishio katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel, wanaendelea kufanyiwa vitendo ya kibaguzi hususan katika wakati huu nyeti ambapo jamii ya kimataifa ipo katika mchakato wa kujaribu kuutafutia ufumbuzi mgogoro kati ya Israel na Palestina.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 287440
Umoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uache tabia zake za kibaguzi dhidi ya raia wa asili nyinginezo waishio katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.