Osama Juwali amesema kuwa mahakama ya ICC haitahusishwa katika kesi ya Saiful Islam na kusisitiza kuwa mwana huyo wa Gaddafi atahukumiwa ndani ya Libya ambako ndiko alikotendea jinai zake. Waziri wa Ulinzi wa Libya amesisitiza kuwa Saiful Islam alifanya jinai ndani ya Libya na anapaswa kuhukumiwa na Walibya wenyewe.Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na jumuiya za kutetea haki za binadamu za nchi za Ulaya na Marekani zinashinikiza Saiful Islam Gaddafi akabidhiwe kwa mahakama ya ICC, suala ambalo linapingwa na viongozi wa Tripoli.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 289047
Waziri wa Ulinzi wa Libya amekosoa uingiliaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) katika kadhia ya kesi ya mwana wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Saiful Islam Gaddafi na kusisitiza kuwa anashikiliwa mahala salama.