19 Machi 2011 - 20:30

Shekh hamd bin khalifah ali thani(Amiri wa Qatar) alie safiri kwenda moritaniya kwa mazungumzo na Raisi wan chi hiyo arejea bila ya mafanikio.

Gazeti la Siraj la Moritaniya laandika: mazungumzo ya Amiri wa Qatar na Raisi wa Jamhuri ya Moritaniya yamepelekea kukasirishwa kwa Raisi wa moritaniya, na sababu iliopelekea kukasirishwa huko ni kwamba, Amiri wa Qatar alimtaka Raisi huyo arekebishe serekari yake na kumuomba kuzidishiwa vikwazo Basharul Asad  (Raisi wa siriya) ili aachene na siasa zake, Raisi wa Moritaniya hakuridhishwa na hilo na kumueleza kuwa yeyey yuko pamoja na Raisi wa Siriya, ama kuhusiana na matukio yanayo  shuhudiwa katika Nchi hiyo alisea kuwa: hakuna chochote zaidi ya Fitina na uadui dhidi ya Serekari ya siriya.
  Taarifa za baadhi ya viombo vya habari vinaelza kuwa: kutokana na misimamo na tofauti zilizotokea baina ya Amiri wa Qatar na Raisi wa Jamhuri ya Moritaniya zilipelekea mjadala mkubwa bainayao na  kutofikia tija yoyote ya safari yake hiyo, pia inasemekana msafara wa Qatar umekataa kupigwa picha na waandishi wa Habari walipokuwa uwanja wandege wakiondoka nchini humo.