Uamuzi wa kupeleka muswada huo wa mwaka 2012 katika mkutano wa sita wa Baraza la Wawakilishi unoanza leo, umekuja baada ya wananchi wengi kutaka wakuu wa taasisi nyeti za dola waidhinishwe na bunge na siyo kuteuliwa na Rais moja kwa moja.Zanzibar haitumii haina sheria ya kuzuia kama ilivyo Tanzania bara ambayo ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).Katika muswada huo, utakaosomwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora unapendekeza adhabu kali ikiwamo faini na kifungo kisichopungua miaka miwili kwa viongozi au watendaji watakaohusika na vitendo vya rushwa.Sehemu ya muswada huo pia umefafanua kwamba, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo baada ya kuteuliwa hataweza kuondolewa na Rais kwani atakuwa amepewa hadhi kama ya Jaji Mkuu ambaye akiteuliwa hawezi kuondolewa.Mkurugenzi huyo atakuwa na mamlaka ya kuchunguza na kumakamata kiongozi yeyote au mtendaji atakayehusika na rushwa.Mkurugenzi huyo pia ataweza kuwashughulikia wakuu wa taasisi za serikali na binafsi na kubadili tabia ambazo zinaashiria vitendo vya rushwa katika sehemu zao za kazi.Kwa muda mrefu wanaharakati wa kutetea kuwapo kwa utawala bora Zanzibar, walikuwa wakishindikiza kwa nguvu kubwa, kuanzishwa kwa taasisi ya kusimamania rushwa, lakini kwa sababu zisizoeleweka kutoka serikalini mpaka sasa taasisi hiyo haijaanzishwa.Mbali na muswada huo, pia wajumbe wa baraza hilo watapata tena nafasi ya kuujadili muswada wa sheria za mafao ya viongozi wa siasa.Muswada huo ulikataliwa katika mkutano uliopita kutokana na kile ambacho wawakilishi walidai ni kuwapo kwa kasoro nyingi za kisheria.Katika mkutano huo, maswali 127 kutoka kwa wawakilishi mbalimbali, yataulizwa.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 291477
Gazeti la mwananchi laandika: SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeandaa muswada wa kuanzisha Taasisi yake ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi, ambayo mkuu wake atateuliwa na Rais na kuiidhinishwa na Baraza la Wawakilishi.