Baraka Obama alisema "viongozi wa Iran lazima watambue kwamba itabidi kutumia nguvu za kijeshi ikiwa mbinu zote za kisiasa sitafeli kuisimamisha Iran kuendeleza na mpango wake wa kinyuklia. Obama aliongeza kwa kusema "Ningeomba Israel wawe na subira ili jitihada za kidilpomasia kufanya kazi yake, ikiwemo vikwazo vya kiuchumi ambavyo nafikiria vitafanikiwa na swaala la mazungumzo ya kivita tusiliongelee kwa sasa." Serikali ya Iran bado yaendeleza msimamo wake kuwa:kama matumizi ya Nyuklia kwa njia ya amani ni makosa, basi nchi zote zisimamishe mpango wao wa nyuklia ikiwepo Marekani na Israel na kama si makosa basi nchi zingine pia ziwe na haki ya kutumia teknolojia hiyo yenye manufaa. Pia Iran imeashiria haita sitisha mpango wake na yeyote atakaye jidanganya kuwa anaweza kuikabili Iran kijeshi basi asubiri hasara isiyofidika.
4 Machi 2012 - 20:30
Msimbo wa Habari: 300623
ABNA inatuarifu kuwa: Raisi wa Marekani Barrack Obama amerejea kutoa vitisho vya kuivamia kijeshi Jamhuri ya kiislam ya Iran iwapo itaendeleza urutubishaji wake wa Nyukilia wa njia ya amani