Ripoti ya ABNA-Kifo cha Fatima Zahra ni kifo kamwe hakitosahaulika katika historia ya Uislamu kwani mambo aliyofanyiwa Mtoto wa Mtume(saw) ni ya kusikitisha katika historia Kiislamu, nani aweza kukubali kuwa Mtoto wa Mtume(saw) alivamiwa na kupigwa na kipigo hicho kilisababisha kuporomosha ujauzito wake, ila la kusikitisha tu ni kwamba baadhi ya watu wajaribu kuficha mambo haya na kukanusha mambo yaliotokea katika historia ya Kiislamu.
Historia imeweka wazi nini kilichotokea baada ya kuaga Dunia Mtume(saw), watu hawakuridhika na wema wa Mutme(saw) malipo yake ni kumuondoa kipenzi cha Mtume(saw) Duniani baada ya myezi kadhaa ya kufariki Baba yake Je! Huu ni Uislamu? Fatima alikuwa ni amana kwetu kutoka kwa Mtume(saw) ila sisi hatukuweza kuhifadhi amana hiyo Je! Huu ni Ubinadamu kwa aliekutendea wema?
Ni kwa kila Muislamu kutambua mambo mawili haya:
1-Matakatizo na tabu alopata Mtume kwa ajili yetu wadhifa wetu kwake ni nini!!.
2-Mtume amesema: Atakae muudhi Fatimah atakuwa ameniudhi mimi na atakae ni udhi mimi atakuwa amemudhi Mwenyezi Mungu.
Fahamu ndugu yangu mpenzi kuficha haki si njia kuongoza jamii bali twazidi kujiongezea mzigo mzito mbele ya Mwenyezi Mungu.








