8 Julai 2012 - 19:30

Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa bunge la Libya lilianza jana saa mbili asubuhi kwa saa za huko. Na hadi kufikia saa mbili jioni, zoezi hilo kimsingi lilikamilika, ambapo vituo mbalimbali vya kupigia kura vilianza kazi ya kuhesabu kura. Upigaji kura ulifanyika katika hali ya utulivu, bila ya kutokea matatizo makubwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume kuu ya uchaguzi ya Libya, asilimia 80 ya wapiga kura walijiandikisha na kushiriki kwenye upigaji kura.

Wachunguzi kumi kadhaa wakiwemo wa Umoja wa Nchi za kiarabu na Umoja wa Ulaya walisimamia uchaguzi huo. Matokeo ya mwanzo ya upigaji kura yatatangazwa tarehe 9, na matokeo ya mwisho yatatangazwa tarehe 11.