Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu amehudhuria kikao cha jumuia NAM kwaajili ya kuhutubia katika ufunguzi wa kikao hicho
Kiongozi huyo aliambatana na viongozi wengine akiwemo Ayatullah Hashimiy Rafsanjaniy,DK Ahmad Najad, DK Ally Larijaniy, Ayatullah Amuliy Larijaniy, Ayatullah Hashimiy Shahrudiy, na hujatul Islamu Muhammad Gulpaiganiy.
Kikao cha 16 cha Jumuia ya NAM kilianza siku ya juma pili ambapo walihudhuria wataalamu na mawaziri wa mambo ya nje wa jumuia hiyo, ama siku ya al hamisi na ijumaa watahudhuria viongozi wakuu wa nchi hizo.
Muda mfupi waliingia viongozi hao sehemu iatakayo fanyika kikao hicho wakiwa na misafara yao ambapo walikuwa marais na wasaidizi wao.
Misafara ya maraisi hao ilianza kumiminika na kuingia nchini Iran kuanzia siku ya juma nne akiwemo Rais wa Misri ( Muhammad Mursiy) ambae alishika mamlaka ya utawala wa jumuia hiyo kwa muda wa mika mitatu, katika ufunguzi wa kikao hicho Rais wa Misri ndiye atakaekuwa muhutubu wa pili wa kikao hicho baada ya kiongozi madhamu wa mapinduzi ya Iran, na kwa hutubayake hiyo Rais huyo atakabidhi rasmi uongozi wa mzunguko wa kumi 16 wa jumuia hiyo kwa Rais wa jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Pia katika kikao hicho walihudhuria baadhi ya viongozi wa Iran, akiwemo mku wa jeshi na viongozi wakuu wengine wa kisiasa.