1 Oktoba 2012 - 20:30

Mlipuko wa gruneti uliotokea leo katika kanisa la Polycap mjini Nairobi umesababisha kifo cha mtoto mmoja na wengine watatu kujeruhiwa.

Akizungumza na shirika la habari la China Xinhua, kamanda wa polisi wa mkoa Moses Ombati amefafanua kuwa shambulizi hilo lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa ni magaidi limetokea saa 4.30 asubuhi na kuwalenga watoto waliopo katika shule ya Jumapili. Aidha amesema polisi imeanza msako mkubwa kwa watu hao wanaoshukiwa kuwa ni magaidi, na pia imeanza uchunguzi ili kujua sababu ya shambuliz hilo.