Vyanzo muhimu vya habari katika Serikali ya Somalia siku ya jumamosi vimtangaza kuwa: Rais wa Jamhuri ya Somalia amemtangaza Abdiy faraj kuwa ni waziri mkuu wa Somalia.Abdiy ni miungoni mwa wafanya biashara wakubwa nchini humo ambae hapo mwanzo hakuwa anafahamika na wananchi hata taasisi za nchi hiyo.Vyanzo hivyo vimetangaza kuwa: Hasan Sheikh Mahmud, Rais wa Jamhuri ya Somalia mwezi uliopita alichaguliwa na wabunge wa nchi hiyo, uchaguzi ambao ulionyesha kuwa anaungwa mkono na umoja wa mataifa.Abdiy ni miungoni mwa watu wakaribu sana kwa Rais wa Jumhuri ya Somalia, naye nikatika wakazi wa mji wa Gadu uliopo kusini mwa magharibi mwa nchi hiyo, naye ni miungoni mwa waitimu waliosoma katika chuo kikuu cha Mugadishu, naye tokea alipo maliza masomo chuoni hapo mpaka sasa nizaidi ya miaka 20 alikuwa mjini Nairobi nchini Kenya akijishughulisha na masuala ya biashara.
6 Oktoba 2012 - 20:30
Msimbo wa Habari: 354406
Rais wa jamhuri ya Somalia amtangza waziri mkuu mpya (Abdiy faraj shardun) ambae ni miungoni mwa wafanya biashara maarufu ambae wananchi hawakuwa wanamfahamu hapo kabla