Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Habari zinazoeleza kuagizwa sms za ushindi wa Hizbullah ndani ya nchi ya Israel, na wakazi wa Lebanon na Israel wathibitisha hilo kwa kuonyesha sms hizo.
Kwa mujibu wa ripoti hii, baada ya kuingia ndege hiyo ya kijasusi ya Hizbullah Sayyid Hasan Nasrullah alieleza kuwa ndege hiyo imetengenezwa na Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran, na lengo la ndege hiyo ni kuingia sehemu ya adui bila kujua au kuonwa na radari.
Ndege hiyo ilizunguuka ndani ya Israel kwa muda masaa matatu na kupiga picha kila sehemu muhimu za Israel, na baada ya kazi nzuri kama hiyo ilikuja hatua ya pili nayo ni kutanzaga ushindi wa Hizbullah kwa njia ya sms kwa Lugha ya Kiarabu na Kiibrania kwa kila mkazi wa Quds na wakazi wa walowezi (Mazayuni) walishuhudia sms za Hizbullah zinazotangaza ushindi.
Na sms yenyewe ni hii: KARIBUNI KATIKA SHIRIKA LA NDEGE LA HIZBULLAH NAMBA MOJA LINALOELEKEA QUDS.
