Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Mwaka wa Mawindo wa ndege za kijasusi za Marekani katika anga la Iran, Jeshi la Iran baada ya kufaanikiwa kunasa ndege ya kijasusi ya Marekani RQ170 leo hii pia Jeshi la Majini la Jamuhuri ya Kiislam ya Iran limenasa ndege nyengine ya kijasusi ya Marekani itwayo Scan Eagle NQ1 katika Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf).

Mara kadhaa ndege za kijasusi za Marekani zilikua zikikusanya ripoti tofauti katika anga ya Jamuhuri ya Kiislam ya Iran na kila zilipokua zikikaribia katika anga la Iran zilikua zikishambulia na Jeshi la Jamuhuri ya Kiislam ya Iran.
Ndege hii imetengenezwa na Shirika Ndege la Boeing, Na ndege hii mwazo ilikuwa ikitumiwa katika kulinda Bahari na kudhibiti uvuvi haramu ila baada ya kupita miaka na kuzidishiwa teknolojia ndege hiyo ilianzwa kutumiwa na Jeshi la Majini la Marekani katika masuala ya kijasusi.

Ndege hiyo ilotengenezwa na Shirika la Boeing baada ya kuongezewa teknolojia ilitumiwa katika vita ya Iraq mwaka 2004 kudhibiti maeneo tofauti ya kivita nchini Iraq.
Ndege hiyo isiyo na rubani Scan Eagle NQ1 inayo kamera iloendelea inayoweza kupiga picha usiku na inauwezo wa kuwasiliana kilometa 100 na sehemu ilotumwa, Aidha inauwezo wa kukaa angani masaa 20.

Scan Eagle NQ1 inarefu wa mita 1.19, Unene wa mita 3.05, Mbawa mbili na uzito wa kilogramu 18, Aidha haihitaji sehemu kubwa ya kuruka, Hutumiwa jeki na kamba ya kuvuta jeki hiyo kwa ajili ya kurushwa, Spidi ya Scan Eagle ni kilometa 120 kwa saa moja.
Mwezi ulopita pia ilishambuliwa vikali ndege isiyo na rubani ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf) na kulazimika kurudi nyuma.
Kulinga na ripoti hii, Serikali ya Jamuhuri ya Kiislam ya Iran imeagiza barua rasmi Umoja wa Mataifa kushitaki mambo yanayofanywa na Marekani kuchupa mipaka ya nchi hiyo.
